MAZUNGUMZO KWA WALE WANAOSITASITA KUPATA CHANJO…na wale wanaowapenda

“Katika janga hili lote lengo letu limekuwa kuwatumia wasanii ili kutusaidia kuelewa nyakati hizi za sisizo za kawaida. Kwa hivyo, wakati Dr. Peter Centre ilipotufikia kuhusu kufanya kazi katika mradi kuhusu watu wanaositasita kupata chanjo, ilitubidi kusema ndiyo — kwa sababu tunaona kwamba suala la chanjo linagawanya marafiki, familia na jamii. Kama wasanii tunataka kufanya sehemu yetu kuleta watu pamoja, na kupigana na kile tunachoona kama athari mbaya zaidi ya janga hili — mafarakano na migawanyiko inayoibuka katika sehemu nyingi za jamii.

Pamoja na Majadiliano ya Wanasitasita Kupata Chanjo na Wale Wanaowapenda, tuliagiza waandishi wanne wa tamthilia ambao mambo waliyokuwa wamepitia maishani yangeweza kutoa maarifa na uelewaji kuhusu baadhi ya hali ngumu zaidi ambazo sote tunakabili.

Tunafikiria haya kama mazungumzo ya kuigiza yanayojumuisha hali ngumu ambazo wengi wetu tunajikuta ndani yake. Iwe ni mjadala unaofanya pamoja nawe mwenyewe, au mtu fulani katika mduara wako, tunatumai michezo hii mifupi itakusaidia kuabiri suala hili kwa fadhili na huruma.”

SHERRY J YOON
Artistic Director
Boca del Lupo

JAY DODGE
Artistic Producer
Boca del Lupo

 KUHUSU BOCA DEL LUPO

Dhamira ya Boca del Lupo ni kutayarisha maonyesho yasiyo ya kawaida katika nafasi zisizo za kawaida. Kampuni imejitolea kwa ufikivu na inafanya kazi kupanua ushiriki, mtazamo na umuhimu wa utendaji wa kisasa ndani ya wingi wa tamaduni za Kanada. Ikiongozwa na Artistic Director Sherry J. Yoon na Artistic Producer Jay Dodge, Boca del Lupo imetengeneza zaidi ya kazi 60 mpya tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1996. Michezo ambayo kampuni hiyo imetayarisha imeonyeshwa kitaifa na kimataifa na kampuni inaandaa programu mahiri ya ukuzaji wa wasanii inayojulikana kama SLaM. Wakati wa usimamizi wa hao wawili, kampuni imepokea tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na Jessies for Outstanding Design, Outstanding Production, Significant Artistic Achievement na Outstanding Performance; Critic’s Choice Award for Innovation; Alcan Performing Arts Award na The Patrick O’Neill Award, ambayo ilishinda kwa Plays2Perform@Home, mradi wa ukumbi wa maonyesho wa nyumbani ambao ulihamasisha Mazungumzo hayo kwa wale Wanaositasita Kupata Chanjo na Wale Wanaowapenda.

Boca del Lupo inashukuru kutayarisha na kufanya kazi kwenye eneo lisilojulikana la watu wa xwm θkw y̓ m (Musqueam), Skwxwú7mesh (Squamish), na S lí̓ lw taɬ (Tsleil-Waututh).

Bocadellupo.com

If you have any thoughts or feedback on this website or the Dialogues, email us at info@bocadellupo.com

Subscribe to our newsletter to stay current on all our projects, workshops, on-going presentations, initiatives & other events.